Wednesday, 21 May 2014

May 21, 2014 10:16 am 0

Picha: Mwili wa marehemu Adam Kuambiana ulivyoagwa viwanja vya Leaders jijini Dar….


ku2
ku1
ku3
ku4
ku6
ku7
ku8
ku9
ku11
ku12
ku14
ku15
ku18

Huku watu wakizimia makaburini,Kuambiana azikwa na maswali magumu matano….


ADAM Philip Kuambiana amezikwa jana kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku akiacha maswali magumu matano kuhusu maisha, mazingira na hatimaye kifo chake, Risasi Mchanganyiko linakupa moja kwa moja.
Marehemu Kuambiana alifariki dunia Jumamosi iliyopita asubuhi akikimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua tumbo ghafla.
ku4
Mwili wa marehemu Kuambiana ukiwasili kaburini tayari kwa shughuli za kuusitiri.
MANENO KUTOKA KWENYE MIDOMO YA WATU
Baada ya kifo chake, maneno kutoka kwenye vinywa vya watu yalionesha ni maswali magumu ambayo majibu yake yangepatikana kama marehemu angekuwa hai.
Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko lilifanya kazi ya ziada kuhakikisha maswali hayo yanapata majibu kwa ndugu au watu wa karibu na marehemu.
MASWALI MAGUMU MATANO
Maswali ya watu kuhusu marehemu Kuambiana yako matano ambayo baadhi ya wasomaji walitoa ombi kwa Magazeti Pendwa ya Global kuyafanyia kazi na kutoa majibu yake kwa vile uwezo huo kwa Global upo.
SWALI LA KWANZA
Inadaiwa kuwa asubuhi ya kifo chake, marehemu na wasanii wenzake walikuwa kambini, Sinza jijini Dar. Wasanii hao walimgongea mlango kwa sababu walitakiwa kwenda kurekodi filamu wakakuta mlango uko wazi, wakaingia.
Je, ni kwa nini marehemu aliacha mlango wazi wakati kuna maelezo kwamba alikuwa akilala na vifaa vingine vya kufanyia kazi?
Stara Thomas ambaye amewahi kuwa mchumba wa marehemu, anajibu hili:
“Ninavyojua mimi Kuambiana alikuwa anavuta sana sigara. Mara nyingi akitaka kuvuta alikuwa akitoka nje. Sasa huenda alfajiri ya siku hiyo alifungua mlango akatoka kuvuta aliporudi hakuufunga tena.”
kuambiana
Adam Philip Kuambiana enzi za uhai wake.
SWALI LA PILI
Yapo madai kwamba, siku hiyo marehemu alikuwa na fedha nyingi. Hilo linaweza kuthibitishwa na rafiki wa karibu wa marehemu ambaye alisema kuwa, Ijumaa, yaani siku moja kabla ya kifo, Kuambiana alikuwa na fedha nyingi.
Kuhalalisha hilo, hata mhasibu wa Gesti ya Silvarado, Sinza jijini Dar ambayo marehemu na wasanii wake waliitumia kupiga kambi kwa ajili ya kurekodia filamu alisema walikuwa wakimdai shilingi milioni mbili na siku hiyo ya Ijumaa alilipa keshi.
Swali ni je! Kama marahemu alikuwa na fedha nyingi japokuwa hakijajulikana kiasi, baada ya kifo chake zilichukuliwa na nani na ameziweka wapi?
NDUGU WA MAREHEMU ANAJIBU
Ndugu wa marehemu ambaye alisema si msemaji wa familia na akaomba jina lake lisitajwe, alisema anachojua yeye marehemu hakukutwa na hata senti tano mfukoni.
“Hilo la kusema alikuwa na fedha siku hiyo hata sisi tunasikia tu. Lakini sisi kama familia tunajua hakukutwa na pesa licha ya kwamba tumesikia alikuwa akiwapa ofa watu kwenye mabaa. Kuna mtu nasikia alitoweka nazo, tunamsaka kila kona.”
SWALI LA TATU
Wengi wanatatizwa na makazi ya marehemu kwamba mtu angetaka kumpata Kuambiana angekwenda wapi maana mara nyingi alikuwa akionekana kwenye baa mbalimbali za jijini Dar hasa maeneo ya Sinza.
“Mimi nimewahi kusikia kwamba, Kuambiana alikuwa hana makazi. Alipokutana na Stara Thomas ndiyo akawa anaishi kwake, walipomwagana ikawa mwendo ni uleule.
“Nimewahi kusikia kuwa alipokuwa akipewa tenda ya filamu ndiyo makazi yake yalikuwa kambini. Lakini sina hakina sana makazi yake japokuwa  na mimi ni msanii wa filamu kama alivyokuwa yeye,” alisema mwigizaji mmoja akiomba asindikwe gazetini.
STARA ATAJA MIKOCHENI
Risasi Mchanganyiko lilizungumza tena na Stara ambaye alijibu:
“Mimi aliniambia makazi yake yalikuwa Mikocheni (Dar) lakini sikuwahi kufika. Lakini ninavyojua ni Mikocheni.”
Akizungumza na gazeti hili msibani kwa mke wa marehemu, Bunju jijini Dar, ndugu mmoja alisema anavyojua yeye marehemu alikuwa akiishi Bunju B.
SWALI LA NNE
Baadhi ya mastaa walisikika wakisema baada ya kuachana na Stara, marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii wa filamu anayeitwa Lulu Jumanne ‘Selina’ Lakini swali likawa je, ni kweli?


mambo hadharan LAMSAKA, LAMPATA SELINA
“Ni kweli mimi na Kuambiana tulikuwa wapenzi. Baada ya kuachana na mke wake wa ndoa (Janeth) alikuja kwangu tukaishi wote, lakini baadaye tukaachana, nikasikia yuko na Stara.
“Hata hivyo walikorofishana na kurudi tena kwangu,” alisema Selina ambaye ndiye mpenzi wa marehemu hadi kifo chake.
SWALI LA TANO
Swali la tano ni kuhusu filamu aliyokuwa akiishuti marehemu ambayo kaiacha katikati inayoitwa Jojo. Marehemu alisema ni yake lakini kuna madai kwamba, Stara Thomas naye anadai ni ya kwake.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka Stara juzi kuhusu madai hayo ambapo alisema:
“Mimi sina tatizo, kama marehemu alisema ni yake sawa tu. Ila ilikuwa ya kwetu sote. Hata ikijulikana ni yake sidhani kama ni tatizo.”
AZIKWA
Marehemu Kuambiana alizikwa jana katika Makaburi ya Kinondoni, Dar ikitanguliwa na misa iliyosomwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo aliagwa.
Mastaa kibao walifurika viwanjani hapo lakini wengi waliishiwa nguvu, kuanguka na kupoteza fahamu.

Thursday, 15 May 2014

WEMA, AUNTY wala ‘Panadol’ kujikinga na Ugonjwa Wa DENGUE



Mastaa wa filamu za Kibongo Wema Sepetu na Anty Ezekiel wameonekana wakinywa dawa aina ya panadol ili kujikinga na ugonjwa uliozuka hivi karibuni ambao umeua watu kadhaa na wengine wakiwa mahospitali unaojulikana kama dengue.
Kupitia mtandao wa instagram anty alipost picha wakiwa wameshikilia dawa hizo mikononi wakati wakila bata sehemu Fulani huku wakijiandaa kuzimeza,huku akiandika hivi.. Dengue hili haya twende kazi Panadol time…
Sababu mojawapo inayoweza kuambukizwa ni kuvaa nguo fupi sasa kwa mastaa wanaopenda kula bata huku wamevaa nguo fupi ndiyo wanajikinga kama Anty na Wema.

Mlevi afariki dunia baada ya kunywa VIROBA vingi bila kula chakula.


Michael  Silanda ( 26 )   mkazi  wa  kijiji  cha  Ibindi, tarafa  ya  Nsimbo  wilaya  ya  Mlele  mkoani  Katavi  amefariki  dunia  baada  ya  kunywa  pombe ( Viroba )  aina  ya  Zed  kupita  kiasi  bila  kula  chakula….
Kamanda  wa  polisi  mkoani  Katavi,Kamishna  Msaidizi  Mwandamizi,Dhahiri Kidavashari  amesema  tukio  hilo  limetokea  wiki  iliyopita  majira  ya  saa  sita  usiku  kijijini  hapo…..
Alisema  siku  ya  tukio  marehemu  baada  ya  kuamka  asubuhi  nyumbani kwake  hapo  majira  ya  saa  tano  asubuhi  alielekea  kwenye  baa  ambayo  ilikuwa  ikiuza  vinywaji  vya  aina  mbalimbali  zikiwemo  pombe  kali….
viroba
Alifafanua  kuwa,baada  ya  kufika  kwenye  baa  hiyo  aliwakuta baadhi  ya  wanakijiji  wenzake  wakiwa  wanakunywa  pombe  za  aina  mbalimbali  hali  ambayo  ilimfanya  marehemu  aweze  kujumuika  nao  kwa  kuagiza  pombe  aina  ya  Zed…
Alisema  Michael  aliendelea  kunywa  viroba  kuanzia  muda  huo  kwenye  baa  hiyo  bila  kula  kitu  chochote  hadi  majira  ya  saa  sita  usiku  alipoamua  kurudi  nyumbani  kwake  huku  akiwa  amelewa  pombe  kupita  kiasi….
Baada  ya  kufika nyumbani  kwake  aliingia  ndani  ya  nyumba  yake  na  kulala  bila  kula  chakula  cha  aina  yoyote  na siku  iliyofuata  majira  ya  saa  mbili  asubuhi  ndipo  walipomkuta  Michael  akiwa  amefariki  huku  akiwa  amelala  kitandani  kwake,…..
Kamanda  Kidavashari  alisema  uchunguzi  wa  awali  uliofanywa  kuhusiana  na  tukio  hilo  umebaini  kuwa  kifo  hicho  kimesababishwa  na  marehemu  kunywa  pombe  nyingi  kupita  kiasi  bila  kula  chakula….

AUNT EZEKIEL ADAI TALAKA!


NYOTA wa sinema za Bongo asiyetabirika maisha, Aunt Ezekiel amedaiwa kudai talaka kutoka kwa ndugu wa mumewe Sunday Demonte kufuatia madai kwamba alikasirishwa na manenomaneno yao kwenye vyombo vya habari.

Ntaa wa sinema za Bongo asiyetabirika maisha, Aunt Ezekiel
Kwa mujibu wa chanzo, nyota huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar baada ya kutua toka  Dubai alikodai alikwenda kwa mume wake.
Ilidaiwa kwamba, mara baada ya kutua Bongo, Aunt alikutana na shoga yake mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja na kutonywa kuwa kuna gazeti liliandika habari yake kwamba wakati mumewe akidaiwa kuwa jela, yeye anaponda raha Dubai.
“Aunt aliambiwa kuwa wasemaji wakubwa wa maneno hayo ni ndugu wa mumewe yaani mashemeji na mawifi zake. Wao wamesema watawasiliana na mume wake kule aliko, hata kama ni gerezani, atoe kibali cha ndugu yeyote wa kiume kuandika talaka na kukabidhiwa Aunt kwa vile hana uchungu na matatizo ya mumewe.
AUNT ASHTUKA KWA MANENO YA NDUGU WA MUME
“Taarifa hizo zilimshtua sana Aunt mpaka akaonekana kupaniki, akajibu mapigo kwa kusema ‘niko tayari kwa talaka, kwanza mimi mwenyewe ndiyo naomba wanipe talaka. Kama hao ndugu wanaweza kwenda kwa Demonte wakapewa kibali cha kunipa talaka basi mimi nasema naomba wanipe’ niko tayari,” kilisema chanzo hicho kikimkariri shoga wa Aunt.

Staa wa sinema Aunt Ezekiel akiwa na mumewe wakati wa ndoa yao

SHUTUMA NYINGINE KWA AUNT
Ama kweli ndoa ndoano, Aunt amekuwa akitupiwa shutuma kibao kutoka kwa baadhi ya ndugu wa mumewe (baadhi lakini) kwamba mke huyo wa ndugu yao hana ushirikiano na wanafamilia kama vile kuwatembelea, kuwajulia hali na hata kuwatupia chochote kitu pale anapokuwa amepata.
“Aunt tangu ameolewa mwaka juzi hajawahi kuja kwangu, mimi namwona kwenye filamu tu. Sijui ni kwa nini Demonte alimuona anafaa kuwa mke wake. Lakini kwa vile kupenda ni moyo, sina usemi,” alisema ndugu huyo ambaye aliomba asichorwe gazetini.
AUNT ASAKWA
Juzi, Amani lilimtafuta Aunt kwa njia ya simu yake ya mkononi ili ajibu madai hayo lakini hakupatikana hewani.Baadhi ya watu wake wa karibu waliliambia gazeti hili kwamba Aunt huwa hapatikani kwenye simu kuanzia saa kumi alfajiri hadi mchana unaofuatia kwa sababu akisharudi nyumbani na kulala huamka mchana jua likiwa utosini.
Mapaparazi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala na kuambiwa hakuwepo na msichana aliyekutwa kwenye makazi hayo.
Amani: Hayupo kasafiri au?
Msichana: Hayupo tu!
Amani: Kuwa muwazi basi.
Msichana: Kwani kusema Aunt hayupo ni usiri?
Baada ya waandishi wetu kuondoka, ilibainika kwamba Aunt ana tabia ya kulala nje, kama si kwa staa mwenzake Wema Sepetu (Mwananyamala, Dar) basi kwa shoga yake kipenzi, Nice Chande (Changanyikeni, Dar).

Amani lilimwendea hewani kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini iliita kwa muda bila kupokelewa. Ilikuwa saa 9:25 alasiri.
Baada ya dakika tano, Amani lilimpigia tena ambapo alipokea. Baada ya salamu, madai yakaanza.
Amani: Inasemekana umedai talaka kutoka kwa mume wako baada ya kusikia manenomaneno kutoka kwa mashemeji zako halafu swali jingine…
Aunt: Sitaki jamani sitaki. Ndoa yangu naomba ipumzishwe. Kwanza naomba kusema kwamba, mimi sijasema kama nimepewa talaka au sijapewa. Ni uamuzi wangu kusema.
“Kwa sasa sijasema lolote, siku nikitaka nitasema. Kwani mimi ndiyo nitakuwa wa kwanza kupewa talaka? Hebu nipumzisheni. Andikeni kuhusu filamu zangu.”
Amani: Filamu yako ipo?
Aunt: Siku ikitoka.
Amani: Basi siku ikitoka tuambie tutaandika.

DIAMOND AINGIA KUGOMBANIA TUNZO ZA BET {Best International Act}

Televisheni kubwa ya Marekani yamchagua Diamond kuwania Tuzo ya Msanii bora wa Kimataifa

Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameipa ten heshima kubwa bendera ya Tanzania kwa kuwa kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa [Best International Act ], Hii na hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma alitangazwa kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards).
Diamond Platnumz kwenye kipengele hichi cha tuzo kubwa za Television kubwa ya burudani Marekani ya BET  yupo kama Best International Act Africa na anawania tuzo hii na wasanii Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka South Africa, Tiwa Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie kutoka Ghana.
BET imetumia twitter kutoa hii taarifa kama kuthibitisha uchaguzi wa Diamond na kuumpa hongera kama msanii pekee  Africa Mashariki.

AVUNJA NDOA YAKE KISA KUIGA MAISHA YA WEMA

Kuiga  ni  kawaida  kwa  wengi.Wapo  walioiga  mambo  fulani  na   hatimaye  wakafanikiwa, na  pia  wapo  walioiga  vitu  flani  wakaharibikiwa.Huyu  aliiga  na  akaharibu  kila  kitu…
Ni  msanii  wa  siku  nyingi  katika  fani.Alitamba  zaidi  akiwa  Kaole, na  hata  mwanzoni  mwa  ujio  wa  filamu  za  Kanumba  alizidi  tu  kashaini….
Kiasili  ni  mweusi  japo  siku  hizi  kuna  weupe  fulani  katika  ngozi  yake  nyororo.Ana  sura  nzuri  yenye  mvuto,umbo  aslia  la  kibantu,meno  yake  meupe  yamepambwa  na  mwanya  mdogo  na  kufanya  iwe  fahari  kumuona  akitabasamu…
Wema Sepetu ‘Madam’.
Wema Sepetu ‘Madam’.

Hana  kashfa  ya  kuvaa  nguo  fupi  sana  ila  aliwahi  kukumbwa  na  skendo  kubwa  zaidi.Mkumbuke  vizuri.Mrefu  wa  wastani,anajua  kutembea,anaongea  kwa  mapozi  huku  akipenda  kulamba  papi  ya  midomo  yake. Umemjua???….Hapana, siyo  huyo…!!
Huyu  ni  mpole  kiasili  na  anapendwa  sana  na  mama  yake.Katika  maigizo  ana  uwezo  wa  kukufanya  uamini  unachoangalia  ni  kitu  halisi.Japo  huwezi  kumtaja, ila  ndani  ya  wasanii  kumi  anapaswa  kuwamo…
Na  ingawa  mvuto  wake  umepungua  kiasi,ila  bado  mrembo  sana.Lakini  wakati  anaigiza  Kaole  alikuwa  mrembo  zaidi.Kwa  uzuri  wake ,  alivuma  na  kila  habari  inayohusu  mwanaume  maarufu  na  mwenye  pesa
Habari  ya  kutakiwa  na  kila  mwanaume , wenye  rangi  na    vipato  tofauti  zilisikika  kila  kona.Baadhi  alitoka  nao  na  wengine  haikuwa  bahati  yao….
Toka  kitambo  almanusura  aolewe, ila  ni  miaka  ya  juzi juzi  ndipo  aliolewa.Uzuri  wake  si  wa  kutafuta, kila  mwenye  macho  na  ngozi  ya  kuhisi  atautambua….
Mbali  na  majanga  yote  aliyopitia  katika  maisha  yake,mengine  yakibaki  kumchafua  na  watu  kudhani  hawezi  kuolewa  na  mwanaume  yeyote  kabla  ya  ile  bahati  ya  mtende  akaolewa; yeye  aliamua  kuachana  na  ndoa  yake  kwa  kuona  aishi  katika  umaarufu  wake….
Mara  kadhaa  alikuwa  akiwaambia marafiki  zake  kuwa, mwenye  hadhi  na  anayetakiwa  kuishi  kama  Wema  Sepetu  sio  Wema  bali  ni  yeye  na  wakongwe wengine  waliosotea  sanaa  na  kuipigania  kama  roho  zao  na  kuilinda  kama  mboni  ya  jicho  lao…..
Akaona  ndoa  sio  mahala  pake,bila  sababu  za  msngi  akaamua  kumwambia  mumewe  watengane….Japo  haikuwa  rahisi ,lakini  walitengana!!
Cha  kufurahisha  ni  kwamba  bado  Wema  anaishi  kama  Wema  na  bado  yeye  haishi  kama  Wema  Sepetu  na  ndoa  haipo  tena…Umemjua  ninayemzungumzia?