Thursday, 15 May 2014

DIAMOND AINGIA KUGOMBANIA TUNZO ZA BET {Best International Act}

Televisheni kubwa ya Marekani yamchagua Diamond kuwania Tuzo ya Msanii bora wa Kimataifa

Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz ameipa ten heshima kubwa bendera ya Tanzania kwa kuwa kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa [Best International Act ], Hii na hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma alitangazwa kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards).
Diamond Platnumz kwenye kipengele hichi cha tuzo kubwa za Television kubwa ya burudani Marekani ya BET  yupo kama Best International Act Africa na anawania tuzo hii na wasanii Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka South Africa, Tiwa Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie kutoka Ghana.
BET imetumia twitter kutoa hii taarifa kama kuthibitisha uchaguzi wa Diamond na kuumpa hongera kama msanii pekee  Africa Mashariki.

0 comments:

Post a Comment