Kuiga ni kawaida kwa wengi.Wapo walioiga mambo fulani
na hatimaye wakafanikiwa, na pia wapo walioiga vitu flani
wakaharibikiwa.Huyu aliiga na akaharibu kila kitu…
Ni msanii wa siku nyingi katika fani.Alitamba zaidi akiwa
Kaole, na hata mwanzoni mwa ujio wa filamu za Kanumba alizidi
tu kashaini….
Kiasili ni mweusi japo siku hizi kuna weupe fulani katika
ngozi yake nyororo.Ana sura nzuri yenye mvuto,umbo aslia la
kibantu,meno yake meupe yamepambwa na mwanya mdogo na kufanya
iwe fahari kumuona akitabasamu…
Wema Sepetu ‘Madam’.
Hana kashfa ya kuvaa nguo fupi sana ila aliwahi kukumbwa
na skendo kubwa zaidi.Mkumbuke vizuri.Mrefu wa wastani,anajua
kutembea,anaongea kwa mapozi huku akipenda kulamba papi ya
midomo yake. Umemjua???….Hapana, siyo huyo…!!
Huyu ni mpole kiasili na anapendwa sana na mama
yake.Katika maigizo ana uwezo wa kukufanya uamini unachoangalia
ni kitu halisi.Japo huwezi kumtaja, ila ndani ya wasanii kumi
anapaswa kuwamo…
Na ingawa mvuto wake umepungua kiasi,ila bado mrembo
sana.Lakini wakati anaigiza Kaole alikuwa mrembo zaidi.Kwa uzuri
wake , alivuma na kila habari inayohusu mwanaume maarufu na
mwenye pesa
Habari ya kutakiwa na kila mwanaume , wenye rangi na vipato
tofauti zilisikika kila kona.Baadhi alitoka nao na wengine
haikuwa bahati yao….
Toka kitambo almanusura aolewe, ila ni miaka ya juzi juzi
ndipo aliolewa.Uzuri wake si wa kutafuta, kila mwenye macho na
ngozi ya kuhisi atautambua….
Mbali na majanga yote aliyopitia katika maisha yake,mengine
yakibaki kumchafua na watu kudhani hawezi kuolewa na mwanaume
yeyote kabla ya ile bahati ya mtende akaolewa; yeye aliamua
kuachana na ndoa yake kwa kuona aishi katika umaarufu wake….
Mara kadhaa alikuwa akiwaambia marafiki zake kuwa, mwenye
hadhi na anayetakiwa kuishi kama Wema Sepetu sio Wema bali ni
yeye na wakongwe wengine waliosotea sanaa na kuipigania kama
roho zao na kuilinda kama mboni ya jicho lao…..
Akaona ndoa sio mahala pake,bila sababu za msngi akaamua
kumwambia mumewe watengane….Japo haikuwa rahisi ,lakini
walitengana!!
Cha kufurahisha ni kwamba bado Wema anaishi kama Wema na
bado yeye haishi kama Wema Sepetu na ndoa haipo tena…Umemjua
ninayemzungumzia?






0 comments:
Post a Comment